Monday, 7 March 2016

JE UNAPENDA UJASIRIAMALI? Soma hapa.

TABIA/SIFA ZA (M)UJASILIA MALI

MAANA YA UJASIRIAMALI

Ujasilia mali nini au Nini maana ya Ujasiriamali?.
Kwa kifupi Dhana ya Ujasiriamali ina maana pana , miongoni mwahizo ni;  Mjasiriamali ni mtu ambaye ana hamasa kubwa ya kuleta mabadiliko chanya katika hali yake ya kiuchumi/ya kimaendeleo  ambaye ana tabia za kipekee ili kufanikisha azma yake hiyo kwa kujishuhulisha (yaani kujiajiri) ili awe na hali nzuri zaidi kiuchumi.

Pia katika hali nyingine Mjasiriamali anaweza kuwa mtu yoyote ambaye anajishughulisha mwenyewe yani amejiajiri katika sekta au shughuli  fulani mfano: kilimo, ufugaji au biashara, uchukuzi n.k.

Neno Ujasiriamali lina asili ya Kifaransa "Entreprenure" sawa na Kutekeleza/Kufanya shughuli fulani mwenyewe katika uwanja wa kibiashara katika maana rahisi ni sawa na kuanzisha biashara/shughuli ya kujiajiri kwa dhumuni la kujitengenezea kipato.

Pia mitazamo mabali ya wasomi imemuelezea  Mjasiriamali kama mtu ANAYEONGOZA, ANAYEPANGA na ALIYE NA UTAYARI juu ya hatari zozote zinazoweza kujitokeza katika biashara/ shughuli yake husika.

Hivyo mimi naweza kusema Mjasiriamali ni Yule mtu anaye tatua shida/ au matatizoya JAMII ilio mzunguka kwakujitengenezea au kujiongezea kipato Mf: Mjasiriamali  anauwezo wakutambua jamii iliomzunguka in uhitaji wakitufulani au bidhaa au huduma Fulani inpatikana mbali au uhitajiwake nimkubwa lakini upatikanaji nipungufu basi hapo ndipo mjasiliamali anaweza kutatua shida hizo mbili (upungufu au umbali wa bidhaa/huduma)

Historia fupi ya ujasiria mali Tanzania

Dhana  ya ujasiriamali Tanzania imeshika kasi hasa katika karne hii ya 21 licha ya kuwapo duniani kwa muda mrefu. Kimsingi, ujasiriamali Tanzania umeshika kasi miaka ya 2000, hasa kutokana na juhudi za Serikali kuboresha sera na sheria mbalimbali za uchumi kwa mfano, sera ya maendeleo ya biashara ndogo ndogo. Kutokana na hili, tumeshuhudia watu wengi wakijitoa kimasomaso kuanzisha biashara au kufanya shughuli mbalimbali za ujasiriamali.

Je, hao wote ni wajasiriamali halisi?

Tuangalie sifa/tabia za m(u)jasilia mali.

1: Mjasiria ansifa ya Kuthubutu

Hii ni tabia muhimu sana kwa mjasiriamali, hapa tunazungumzia uwezo na utayali wa kufanya MAAMUZI ya kuingia katika BIASHARA  fulani au mradi fulani huku ukiwa umeondoa nidhamu ya woga.  Watu wengi ni waoga wa kuchukua hatua au kuthubutu kuingia katika biashara,mradi n.k,
Watu wanaogopa hasara, hawajui jinsi ya kuendesha  mradi weyewe. Mtu ili aitwe mjasiliamali ni lazima awe na uwezo wa kuhtubutu kufanya jambo, lakini jambo atakalo thubutu kufanya lazima afanye utafiti wa kutosha ili baadaye limletee tija. Waswahili mwanasema? UWOGA NI UMASIKINI?.

2: Mbunifu

Mjasiriamali yoyote ni mbunifu,
 Hapa ninapozungumzia ubunifu ninamaana hii,  je! unapata kitu tofauti kila siku ambacho jamii yako itapendezwa nacho au umeng'ang'ania aina moja siku zote? lazima kama mjasiriamali uwe mbunifu kila siku kuhakikisha unapata njia mpya ambazo zitakufanya upanue soko lako au kazi yako,  hapa Mjasiliamali trough innovation and renovation anaweza kufanya kitu chakipekee nakikavutia wengi katika jamii hivo akajitengenezea kipato)

3: Anapenda kujifunza

Hapa ndipo ugonjwa wa watu wengi ulipo mtu anajiita mjasiriamali lakini muulize kasoma vitabu vingapi vya ujasiriamali au kahudhuria semina ngapi za ujasiriamali watanzania wengi tunapenda sana vitu vya urahisi hatupendi kujifunza kama kweli unataka kuwa mjasiriamali au ni mjasiriamali lazima uwe na sifa hii upende kujifunza kutoka kwa watu wengine na uhudhurie semina au mafunzo mengi ya ujasiriamali lassiivyo utabaki kuwa mfanyabiashara. Yawezekana  Watanzania wengi wesiweze kusoma au kwakisingizio chakukosa Muda basi siombaya hata kudhuria semmina mabarimbari za kijasiria mali hivyo ukaweza kupata maarifa yakukuwezesha kufika mabari kibiashara.

4: Asie ogopa kushindwa na kukata tamaa

Watu wengi hushindwa ktk biashara kwa kuogopa kushindwa anataka kuanzisha kitu lkn cha kwanza anawaza nikifirisikka je watu siwatanicheka? acha mawazo mgando rafiki kama kweli we ni mjasiriamali au unataka kuwa mjasiriamali kamwe usiogope kushindwa kwani ninasema mjasriamali ni mtu ambae yuko tayari kushindwa na kujaribu tena (risk taker) matajiri wote unaowaona duniani wamefeli mara nyingi na ndio wakaja kufanikiwa sasa kama unataka kuwa mjasiriamali usiogope kushindwa na wala usikate tamaa ukishindwa unaanza tena na tena na tena hiyo ndio sifa ya mjasiriamali.

5:Mtu anae tumia Nuda wake wa ziada kufanya kitu cha ziaada.

Siku zote mjasiriamali ni mtu ambaye anauwezo wa kufanyabiashara zaidi ya moja yuko tayali kutumia muda wak wa ziada kufanya kitu ambacho japo kimuingizie hata elfu kumi kwa siku mtu ambaye anauwezo wa kutumia muda wake wa ziada kufanya kitu cha ziada huwa anafanikiwa saana maana huwa hapotezi muda. Usipoteze muda  rafiki maisha yamebadilika, unatumiaje muda wako wa ziada wakati vipo vitu
ambavyo unaweza fanya na kujiongezea kipato,usisubiri kesho anza leo.tumia muda wako wa ziada kuigiza kipato cha ziada.


6: Mtu mwenye mahusiano mzuri na watu mablimbali ya kibiashara.

Watu wengi hawaamini katika nguvu ya mtandao (power of network) kama kweli we ni mjasiriamali lazima uwe na mahusiano mazuri na watu wengi ya kibiashara lakini ukiangalia wajasiriamali wengi leo hii hawana mahusiano mazuri na watu wengine kibiashara hutaweza kukua kibiashara kama hutaweza jifunza kutoka kwa wangine jifunze kutoka kwa wengine rafiki na hutawezajifunza kama hutakuwa na mahusiano mazuri na watu wengi kibiasha.

7: Anapenda Ushindani.

Siku zote kama mjasiriamali usipend kukwepa ushindani shindana ili product yako iwe bora,watu wengi hushindwa kufanikiwa ktk biashara
kwasababu ya kuogopa ushindani,anashindwa kufanyabiashara fulani kwasababu washindani wengi,unapokutana na washindani wengi ndio
unafaham mapungufu yako na yao ukijirekebisha unafanya product yako kuwa bora.

8: Mjasiliamali  ni mtu Anae itumia vizuri Jamii inayo mzunguka kuingiza kipato.

Watu wengi hushindwa kulitambua hili na kujiita wajasiriamali lakini hawajui jinsi ya kuwatumia watu wanaokuzunguka ktk kukuingizia kipato,rafiki unawatumiaje watu ambao mmekutana kwenye kikao cha harusi,kikao cha kitchen part au kikao cha familia au kwenye kahawa ktk kuitambulisha biashara yako au unajua kazi kupiga umbea na kupiga story zisizokuwa na tija tu na kulalamika biashara yako haitoki hupati wateja ,unategemea wateja unawapata wapi kama sio hao.

Amka sasa na ufanye yalio BORA  yawezekana ukawa unategemea kipato cha Ajira mwisho wamwezi  lakini kumbe unaweza kutumia muda waziada nakutengeneza kipato cha ziada zaidi hata ya kile cha mwisho wa mwezi, anza sasa usisubiri Kesho.

Ukiwa unapenda UJASIRIAMALI  basi nakuwekea moja ya pendekezo la  FURSA shughuli zakijasiriamali katika sector ya mawasiliano. Sector inayokuwa kwa kasi Nchini na Duniani, Sectory yenye matajiri  wakubwa  Chini  na Dunia yote kwa ujumlwa , Karibu na  ujiunge sasa na FURSA KUBWA YA BIASHARA ya RIFARO AFRICA fursa inayokuwezesha kutengeza KIPATO cha WIKI na kipato cha MWEZI kisicho na kikomo kwakutumia simu yako ya Mkononi maelezo zaidi  Mawasiliano 0753376495 au 0719064402 au 0625688223.... R347631.

No comments:

Post a Comment