Sunday, 13 March 2016

Hawa ndio wakuu wa MIKOA wapya

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa wakuu
wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara, ambapo kati yao
13 ni wapya, 7 wamebakizwa katika vituo vyao
vya kazi, 5 wamehamishwa vituo vya kazi na 1
amepangiwa Mkoa Mpya wa Songwe.
Uteuzi huo umetangazwa na Kaimu Katibu Mkuu
Kiongozi, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe leo
tarehe 13 Machi, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam.
Wakuu wa Mikoa walioteuliwa ni kama ifuatavyo;

1. Mh. Paul Makonda - Mkuu wa Mkoa wa Dar es
salaam.
2. Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Elias Kyunga -
Mkuu wa Mkoa wa Geita.
3. Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu -
Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
4. Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga -
Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
5. Brigedia Jeneral Mstaafu Emmanuel Maganga
- Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.
6. Mh. Godfrey Zambi - Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
7. Dkt. Steven Kebwe - Mkuu wa Mkoa wa
Morogoro.
8. Kamishna Mstaafu wa Polisi Zerote Steven -
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
9. Mh. Anna Malecela Kilango - Mkuu wa Mkoa
wa Shinyanga.
10. Mhandisi Methew Mtigumwe - Mkuu wa Mkoa
wa Singida.
11. Mh. Antony Mataka - Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu.
12. Mh. Aggrey Mwanri - Mkuu wa Mkoa wa
Tabora.
13. Mh. Martine Shigela - Mkuu wa Mkoa wa
Tanga.
14. Mh. Jordan Mungire Rugimbana - Mkuu wa
Mkoa Dodoma.
15. Mh. Said Meck Sadick - Mkuu wa Mkoa
Kilimanjaro.
16. Mh. Magesa Mulongo - Mkuu wa Mkoa Mara.
17. Mh. Amos Gabriel Makalla - Mkuu wa Mkoa
Mbeya.
18. Mh. John Vianey Mongella - Mkuu wa Mkoa
Mwanza.
19. Daudi Felix Ntibenda - Mkuu wa Mkoa wa
Arusha.
20. Mh. Amina Juma Masenza - Mkuu wa Mkoa
wa Iringa.
21. Mh. Joel Nkaya Bendera - Mkuu wa Mkoa wa
Manyara.
22. Mh. Halima Omary Dendegu - Mkuu wa Mkoa
wa Mtwara.
23. Dkt. Rehema Nchimbi - Mkuu wa Mkoa wa
Njombe.
24. Mhandisi Evarist Ndikilo - Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
25. Mh. Said Thabit Mwambungu - Mkuu wa Mkoa Ruvuma.
26. Luteni Mstaafu Chiku Galawa - Mkuu wa Mkoa wa Songwe (Mkoa mpya).

Wakuu wote wa Mikoa walioteuliwa, wataapishwa
Jumanne tarehe 15 Machi, 2016 saa 3:30 Asubuhi
Ikulu, Jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment