BIASHARA YA RIFARO SIYO UPATU: USIPOTOSHWE NA MTU YEYOTE..
Kumekuwepo dhana potofu nyingi mitaani na mitandaoni kuhusu biashara yoyote ya network marketing!!
Dhana potofu ya kwanza: 1
Wengine wanasema kwamba kwenye biashara ya mtandao kama hii tunayofanya na kampuni ya Rifaro Africa kuwa waliotangulia kujiunga ndio wanaonufaika sana na matunda ya biashara. Huu ni mtazamo hasi. Ni mtazamo wa watu wasiojua kanuni ya multiplication effects na power of team work. Lengo kuu la kuanzisha mfumo huu wa biashara ya mtandao ni kuwezesha business partners kushirikiana kiuchumi.
Mfumo wa network marketing business husaidia mshirika kuendelea kupata kipato hata kama itatokea dharura ya kuugua kwa kipindi kirefu na kushindwa kuzalisha tena.
Mtu aliyeko kwenye biashara hii akiwa na team ya watu zaidi ya 10 haiwezekani watu hao wakaugua wote kwa siku moja au wakafariki wote kwa pamoja na kusababisha kipato kukatika.
Hii ni tofauti kabisaa na mfumo wa kawaida wa biashara tulizozizoea mitaani Kama duka, miradi ya ufugaji, kilimo, nk. Mmiliki akiugua muda mrefu au akipata msukosuko kifamilia na biashara yake hulegea au kufa kabisa!! ??????????????
Ukweli katika biashara kama hii ya mfumo wa Rifaro ni kwamba mtu hulipwa kipato kulingana na bidii yake na siyo muda alioanza biashara au watu aliowaingiza kwenye biashara.
Mfano, kuna mtu alijiunga kwangu mimi lakini kutokana na bidii yake ameshalipwa commission kubwa kunizidi.
Yeye ameweza kuingiza watu zaidi ya 25 na kulipwa zaidi ya shs 500,000 ndani ya siku 50 tu wakati mimi niliyetangulia nimefanikiwa kuingiza watu 10 tu na kulipwa shs 200,000 kwa miezi 2 iliyopita. Kwa hiyo hoja siyo kutangulia kuingia kwenye biashara hoja ni kuielewa fursa hii na kuwa crazy zlioko chini wanawanufaisha wa juu. Kwanza kwenye biashara hii hakuna wa juu au wa chini. Wote tuko level moja na tunafanya kazi kama team.
Katika kampuni hii ya Rifaro Africa kipato cha mtu hutokana na bidii yake ya kuunda team aitakayo mwenyewe kulingana na ndoto yake! Malipo ya kuunda team hulipwa kila wiki.
Msukumo wa kuunda team kubwa mtu anatakiwa aupate kutokana na hizo sababu nilizozitoa awali kwamba ukiwa na team kubwa ya wafanyabiashara wenzako ni nadra sana kutetereka kiuchumi kwani siyo rahisi team nzima kukumbwa na misukosuko kiuchumi kwa wakati mmoja.
Dhana potofu ya pili: 2
Kuna dhana hii potofu sana kwenye Biashara kama hii kuwa ni biashara kama ya UPATU.
Huu ni mtizamo finyu. Ni mtizamo mfinyu wa watu wasiosoma hata makala ya ukurasa mmoja. Wavivu wa kusoma. Wavivu wa kufikiri. Naam, ni mtazamo wa watu wenye Makengeza ya kufikiri kichanya na wanawaza hasi tu.
Biashara ya UPATU au "pyramid scheme " ni tofauti sana na biashara ya mtandao. Watu huchanganya mtandao na piramidi.
Piramidi haiwezekani ikawa mtandao!! Labda watu huchanganywa na maelekezo ya picha itumikayo kufafanua muundo wa biashara.
Biashara ya piramidi huwa haina bidhaa inayouzwa. Rifaro Africa tunauza vocha. Piramidi business huuza pesa na kuzizungusha kwa watu waliotangulia kuingia. Yaani watu wapya wakitoa pesa zinaenda kulipa wale waliotangulia.
Mfano wa kampuni ya biashara ya piramidi hapa Tanzania ilikuwa kampuni ya DECI iliyofungiwa na serikali kufanya biashara hiyo haramu nchini.
Biashara ya kampuni hiyo haikuwa kuuza bidhaa yoyote. Rifaro Africa tunauza vocha!! DECI haikuwa na bidhaa yoyote hata ya kutembeza karanga.
Biashara ya piramidi huwa haina bidhaa yoyote. Biashara yake ni kuchangiana pesa tu. Leo mnamchangia Huyu! Kesho mnamchangia yule!! Mnamchangiana weeeee wala hakuna bidhaa yoyote zaidi ya kuchangiana pesa tu. Hiyo ndo piramidi business.
Kwenye biashara ya Rifaro Africa kwa mfano ukiwa kwenye team au usiwe na team bado unalipwa kulingana na usambazaji wa muda wa maongezi ulioufanya kwa mwezi.
Unayo fursa ya kusambaza au kuuza vocha za mitandao yote mahali popote Tanzania bila kuathiri kazi zako za kila siku na bila kuzuiliwa na mipaka yoyote ya mikoa au mitandao tofauti ya simu!
Unayo fursa ya kulipwa hadi 7% ya vocha zote utakazouza kulingana na kazi zako za kuuza vocha au ukubwa wa team yako.
Dhana potofu ya tatu: 3
Dhana nyingine potofu kuhusu biashara hii ni kwamba biashara hii ni ngumu sana. Wengine husema kuwapata watu wa kujiunga ndiyo tatizo.
Ukweli ulivyo ni kwamba biashara zote duniani kote ni ngumu sana. Ugumu wa biashara yoyote hutokana na aina ya bidhaa na aina ya wateja.
Bidhaa za Rifaro Africa siyo kwamba zinatoka kwa kasi tu zaidi ya bidhaa yoyote nchini bali pia ni bidhaa ambayo kila mtu anaihitaji iwe usiku mchana, kwenye misiba, kanisani, misikitini, safarini, kwenye sherehe, ofisini, mashambani, migodini, nk.
Hakuna bidhaa yoyote nchini inayotembea kama vocha za muda wa maongezi iwe Mjini au vijijini.
Mimi nafanya biashara ya vocha dukani kwangu. Pia nauza bidhaa nyingine nyingi. Nikinunua vocha za shs 150,000 zinaisha ndani ya wiki moja. Lakini nikinunua maji ya kunywa au mafuta ya kujipaka au yale ya kupikia chakula yanamaliza hata miezi 3 hayajaisha.
Kwa hiyo, biashara ya Rifaro Africa inakuwa ndo biashara pekee Tanzania inayouzika sana kuliko bidhaa kama vile kahawa, chai, mafuta ya taa, mafuta ya gari petrol, maji, nguo, nafaka, nk.
Watu wengi zaidi hawajiungi Rifaro Africa siyo kwamba biashara hii hailipi au ni ngumu!! Bali kwa sababu ya uongo mwingiiiiiii uliosambaa mitaani.
Bila Shaka nimekupatia shule ya maana hivyo utaendelea kusajili watu zaidi ili team yako ikue na kipato chako kikue zaidi. Kwa maelezo 0753376495...0719064402 Namba ya Kujisajiria ni R347631www.rifaroafrica.com
No comments:
Post a Comment